Orodha ya Mambo Kadhaa katika Kutokomeza Udhalimu
Migogoro mikubwa zaidi duniani leo si ya kati ya nchi na nchi bali ni ile iliyo ndani ya hizo nchi, ambayo inahusisha wadhalimu dhidi ya watu wanaowakandamiza. Inaaminika kwamba watu hawa wanaonyanyasika wana njia mbili za kuchagua: ama kukubaliana na udhalimu wakiamini kwamba utapungua makali au kuleta uasi kwa njia ya matumizi ya nguvu ili kuleta uhuru. Mtazamo huu unapingwa na ukweli kwamba kampeni za kutumia nguvu ya umma (mara nyingine mavuguvugu ya “nguvu ya umma” au migogoro baridi) zimetokea mara nyingi zaidi kuliko ambavyo inafahamika. Mwanzoni mwa mwaka 1900, kulikuwepo wastani wa kampeni moja kubwa ya matumizi ya nguvu ya umma kumpinga mtawala aliyeko madarakani kwa mwaka. Mavuguvugu haya yanayoongozwa na wananchi yameonesha mara kadhaa matokeo ya migogoro mikubwa ya kijiografia na kisiasa na vipindi vya mpito vya kidemokrasia tangu 1972. Hata hivyo, watunga sera, wanazuoni, waandishi wa habari, na wafuatiliaji wengine wenye mapenzi mema wanaichukulia kawaida tu nguvu ya wananchi wa kawaida kana kwamba haiwezi kupambana na udhalimu na kuleta haki bila kutumia mabavu.
Editors: Mathew Burrows and Maria J. Stephan
The Atlantic Council, Washington, DC — 2015
Translation: JPD Systems, March 2019